Ligi Kuu England

LEO ni Anfield=Liverpool v Tottenham

Jumatatu, 06 Februari 2012 18:32
Chapisha Toleo la kuchapisha

anfieldRATIBA:

Jumatatu, 6 Februari 2012

[Saa 5 Usiku]

Liverpool v Tottenham

MSIMAMO Timu za juu:

[Timu zimecheza Mechi 24]

1 Man City Pointi Pointi 57

2 Man United 55

3 Tottenham [Mechi 23] 49

4 Chelsea 43

-----------------------------------

5 Newcastle 42

6 Arsenal 40

7 Liverpool [Mechi 23] 38

8 Sunderland 33

9 Norwich 32

10 Swansea 30

-----------------------------

Taarifa:

Liverpool wapo kwao Anfield kucheza mechi ya Ligi Kuu England wakiwinda ushindi ili kuipiku Arsenal nafasi ya 6 na kuzisakama Newcastle na Chelsea zilizo juu yao katika ile vita ya kumaliza katika Timu 4 za juu ili kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao lakini wapinzani wao wa leo ni Tottenham waliokamata nafasi ya 3 na ambao bado wana ndoto ya kuwa Bingwa kwa vile wako pointi 6 nyuma ya Manchester United walio nafasi ya pili na pointi 8 nyuma ya vinara Manchester City.

Leo Mchezaji wa Liverpool alietoka kifungo cha mechi 9, Luis Suarez, huenda akacheza na pia Nahodha wao Steven Gerrard pia huenda akacheza baada ya kupumzishwa mechi iliyopita.

Nao Tottenham huenda wakampa namba kwa mara ya kwanza Mchezaji wao mpya Louis Saha hasa kwa vile Mafowadi wao Jermaine Defoe, Emmanuel Adebayor na Rafael van der Vaart wana hatihati kwa kuwa na maumivu.

Mara ya mwisho Timu hizi kupambana ilikuwa Mwezi Septemba huko White Hart Lane na Liverpool kuchapwa mabao 4-0 lakini, mbali ya kuifunga Liverpool bao 2-0 Msimu uliopita Mwezi Mei Mwaka jana Uwanjani Anfield, Tottenham walikuwa hawajashinda hapo katika mechi zao 16 nyingine.

Lakini katika mechi zao 5 za mwisho kukutana, Liverpool wameshinda moja tu na kuchapwa 4.

RATIBA MECHI ZIJAZO:

Februari 11

Saa 9 Dak 45 Mchana

Manchester United v Liverpool

Saa 12 Jioni

Bolton Wanderers v Wigan Athletic

Sunderland v Arsenal

Blackburn Rovers v QPR

Swansea City v Norwich City

Everton v Chelsea

Fulham v Stoke City

Saa 2 na Nusu Usiku

Tottenham v Newcastle United

Februari 12

Saa 10 na Nusu Jioni

Wolves v West Bromwich

Saa 1 Usiku

Aston Villa v Man City

Kutoa maoni

Tafadhali toa maoni sahihi kwa kutumia lugha ya heshima.


Security code
Onyesha tena

Ingia

Jiandikishe / Ingia

adidas

All Originals 300x250

MATANGAZO

Adidas Predator 300x250

TANGAZA HAPA