DIMBANI AFRIKA

SH. 2,000 TU KUONA MECHI YA STARS, DRC

Jumatatu, 20 Februari 2012 16:53
Chapisha Toleo la kuchapisha

TAIFA_STARS-smallTaarifa kutoka kwa Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, Boniface Wambura imesema kiingilio kwa ajili ya mechi ya Kirafiki ya Kimataifa kati ya Taifa Stars na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) itakayofanyika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Alhamisi Februari 23 kitakuwa Sh. 2,000 kwa Viti vya Kijani na Bluu.

Eneo hilo la Viti vya Kijani na Bluu linachukua Watazamaji 36,693 ambao ni karibu theluthi mbili ya Viti vyote kwenye Uwanja huo wa kisasa.

Viti vya rangi ya Chungwa kiingilio ni Sh. 5,000, VIP C itakuwa Sh. 7,000 wakati VIP B tiketi zitauzwa kwa Sh. 10,000.

Kiingilio kwa viti vya VIP A kitakuwa Sh. 15,000.

Kwa vile Februari 23 ni siku ya kazi na ili kutoa fursa kwa Washabiki wengi kushuhudia pambano hilo la Kimataifa, mechi hiyo itaanza saa 11 kamili jioni.

Taifa Stars inayofundishwa na Jan Poulsen imeingia kambini leo na inatarajiwa kuanza mazoezi jioni hii kwenye Uwanja wa Karume na DRC ambayo iko chini ya kocha Claude Le Roy, aliewasili Nchini tangu juzi, inatarajiwa kutua Nchini kesho.

Taifa Stars na DRC zinatumia mechi hiyo kunoa Wachezaji wao kabla ya mechi zao za mchujo za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON2013) zitakazofanyika Mwakani nchini Afrika Kusini.

Katika Raundi ya Awali ambayo mechi zake zitachezwa Februari 29 mwaka huu, Stars itaanzia nyumbani dhidi ya Msumbiji wakati DRC inaanzia ugenini dhidi ya Seychelles.

Kutoa maoni

Tafadhali toa maoni sahihi kwa kutumia lugha ya heshima.


Security code
Onyesha tena

Ingia

Jiandikishe / Ingia

adidas

All Originals 300x250

MATANGAZO

Adidas Predator 300x250

TANGAZA HAPA