DIMBANI AFRIKA

ZAMBIA BINGWA==Renard: ‘Iliandikwa Mbinguni!’

Jumatatu, 13 Februari 2012 18:19
Chapisha Toleo la kuchapisha

HEVRE_RENARD_JUUKocha wa Zambia, Herve Renard, anaamini kuwa ushindi wao wa kushangaza dhidi ya Vigogo Ivory Coast ambao kila mtu alijua ndio Mabingwa watarajiwa wa Afrika kwenye Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2012, hapo jana huko Libreville, Gabon ‘uliandikwa mbinguni’.

Kabla ya Fainali hiyo, Zambia walicheza mechi zao zote za AFCON 2012 Nchini Equatorial Guinea na walitua hapo Mji wa Libreville, Gabon akwa ajili ya mechi ya Fainali tu kwenye Mji mbao katika historia ya Zambia hautasahaulika milele kwani ndio sehemu waliyopata maafa makubwa Mwaka 1993 wakati Ndege iliyobeba Timu yao ya Taifa ilipoanguka na kuwaua Wachezaji wao.

Renard alitamka: ‘Tulitaka kuwapa heshima na kuwaenzi wenzetu waliotangulia mbele ya haki, kuja hapa kwa Fainali ni ishara ya kudra yetu, imeandikwa mbinguni, kulikuwa na nguvu kwetu. Nadhani Mungu alitusaidia na kutupa nguvu kubwa!’

Mara baada ya Zambia kuibwaga Ivory Coast kwa penati 8-7, Renard alikumbatiana na Rais wa Shirikisho la Soka la Zambia, Kalushwa Bwalya, ambae pamoja na mwenzake Charles Musonda ndio walinusurika kwenye ajali hiyo ya Ndege kwa kutolkuwemo kwa vile tu iliamuliwa wasiende Zambia bali wasafiri moja kwa moja kutoka kwenye Klabu zao za Ulaya na kwenda Senegal ambako wangejiunga na wenzao.

Renard, ambae alikuwa Kocha wa Zambia Mwaka 2008 na kuacha ngazi na kurudishwa tena na Kalusha Bwalya kabla ya AFCON 2012, alimshukuru Kalusha kwa kumpa nafasi hii ya sasa.

Kutoa maoni

Tafadhali toa maoni sahihi kwa kutumia lugha ya heshima.


Security code
Onyesha tena

Ingia

Jiandikishe / Ingia

adidas

All Originals 300x250

MATANGAZO

TANGAZA HAPA