DIMBANI AFRIKA

Blatter-Viongozi wa Soka Misri waliofukuzwa warejeshwe!

Jumatatu, 06 Februari 2012 17:07
Chapisha Toleo la kuchapisha

Rais wa FIFA, Sepp Blatter, ametaka Viongozi wote wa Shirikisho la Soka la Misri, EFF, waliotimuliwa na Serikali mara baada ya vurugu kusababisha vifo vya Watu 74 Uwanjani Mjini Port Said mara baada ya pambano la Ligi kati ya Klabu za Al-Masry na Al-Ahly Wiki iliyopita.

Akiongea huko Mji mkuu wa Paraguay, Asuncion, Blatter alisema kufukuzwa kwa Viongozi hao ni kuingiliwa na Serikali kitendo ambacho ni kinyume na kanuni za FIFA na wametaka Viongozi hao warejeshwe madarakani.

Blatter amesema Viongozi hao ni lazima warejeshwe na watawatakawasimamie  maafa kama yaliyotokea huko Port Said yasirudiwe tena.

Hatua hii ya sasa huenda ikasababisha Misri kufungiwa na FIFA ikiwa Serikali itagoma kuwarudisha madarakani Viongozi hao waliofukuzwa na hili huenda likatoa mwanya kwa Yanga ambao wamepangiwa kucheza na Klabu ya Misri Zamalek katika CAF CHAMPIONZ LIGI hapo Februari 18 Jijini Dar es Salaam na marudiano mwanzoni mwa Machi huko Cairo kupata ushindi wa chee.

Hadi sasa huko Misri shughuli zote za Soka zimesimama.

Kutoa maoni

Tafadhali toa maoni sahihi kwa kutumia lugha ya heshima.


Security code
Onyesha tena

Ingia

Jiandikishe / Ingia

adidas

All Originals 300x250

MATANGAZO

TANGAZA HAPA

SOKAINBONGO_BANNER1