Baada ya kuichabanga Namibia kwa jumla ya mabao 7-2, Timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania, Twiga Stars, itacheza na Ethiopia kwenye Raundi ya Kwanza ya michuano ya Kombe la Afrika kwa Wanawake ili kutafuta nafasi ya kuingia Fainali zake ambazo zitachezwa Mwezi Novemba huko Malabo Nchini Equatorial Guinea.
Ethiopia wamefuzu baada ya kuichapa Misri bao 4-0 na kuwatoa kwa jumla ya bao 6-4.
Mechi ya kwanza kati ya Twiga Stars na Ethiopia itachezwa huko Addis Ababa kati ya tarehe 25 hadi 27 Mei 2012 na marudiano ni Nchini Tanzania kati ya tarehe 15 hadi 17 Juni 2012.
MATOKEO KAMILI Mechi za Raundi ya Awali:
Ghana 5 Mali 0
*Ghana wamesonga kwa jumla ya Mabao 8-0
Tanzania 5 Namibia 2
*Tanzania wamesonga kwa bao 7-2
Guinea 0 Cote d’Ivoire 5
*Cote d’Ivoire wamepita kwa bao 10-1
Ethiopia 4 Egypt 0
*Ethiopia wamesonga kwa bao 6-4
Malawi 4 Zambia 2
*Zambia wameshinda jumla ya bao 9-4
Zimbabwe 2 Botswana 1
*Zimbabwe wamepita kwa bao 3-1
DR Congo 4 Uganda 0
*DR Congo wamesonga kwa bao 5-1