DIMBANI AFRIKA

AFCON 2012: Zambia yaichapa Senegal

Jumapili, 22 Januari 2012 07:24
Chapisha Toleo la kuchapisha
AFCON_SIB_LOGO12MATOKEO:

Januari 21

KUNDI A

Equatorial Guinea 1 Libya 0

Senegal 1 Zambia 2

RATIBA:

Januari 22

KUNDI B

Ivory Coast v Sudan [Saa 1 Usiku]

Burkina Faso v Angola [Saa 4 Usiku]

TAARIFA:

Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON, zinazochezwa huko Nchini Gabon na Equatorial Guinea, zilianza jana kwa mechi za Kundi A na Wenyeji Equatorial Guinea kuifunga Libya bao 1-0 na Zambia kuiangusha Senegal, Timu iliyopewa nafasi kubwa Senegal, mabao 2-1.

Bao za Zambia, maarufu kama Chipolopolo, zilifungwa na Emmanuel Mayuka dakika ya 12 na Rainford Kalaba dakika ya 20.

Senegal, ikicheza wakiwa na Straika tishio kutoka Newcastle Demba Ba, walipata bao lao pekee dakika ya 74 alilofunga Dame Ndoye alieingizwa toka benchi.

Nao Wenyeji Equatorial Guinea ambao wengi hawawapi matumaini waliifunga Libya bao 1-0 kwa bao pekee la Javier Balboa katika dakika ya 87.

Mechi zijazo kwa Kundi A ni hapo Januari 25 Libya v Zambia na Equatorial Guinea v Senegal.

MAKUNDI & RATIBA

MAKUNDI:

Kundi A: Equatorial Guinea, Libya, Senegal, Zambia

Kundi B: Ivory Coast, Sudan, Burkina Faso, Angola

Kundi C: Gabon, Niger, Morocco, Tunisia

Kundi D: Ghana, Botswana, Mali, Guinea

Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitachezwa kuanzia Januari 21, 2012 na kumalizika Februari 12, 2012 Nchini Equatorial Guinea na Gabon.

Mechi ya ufunguzi itakuwa ni kati ya Wenyeji Equatorial Guinea na Libya hapo Januari 21, wote wakiwa Kundi A pamoja na Senegal na Zambia, na itachezwa Mjini Bata huko Equatorial Guinea.

Wenyeji wenza wa Equatorial Guinea, Gabon, wao wapo Kundi C na watacheza Mjini Libreville, Gabon wakiwa pamoja kwenye Kundi hilo na Niger, Tunisia na Morocco.

Kundi B watacheza mechi zao Mji Mkuu wa Equatorial Guinea, Malabo, na zipo Nchi za Ivory Coast, Sudan, Burkina Faso na Angola.

Kundi D litakuwa Mji wa Franceville, Gabon na zipo Ghana, Botswana, Mali na Guinea.

RATIBA/MATOKEO:

[Saa za Bongo]

Januari 21

KUNDI A

Equatorial Guinea 1 Libya 0

Senegal 1 Zambia 2

Januari 22

KUNDI B

Ivory Coast v Sudan [Saa 1 Usiku]

Burkina Faso v Angola [Saa 4 Usiku]

Januari 23

KUNDI C

Gabon v Niger [Saa 1 Usiku]

Morocco v Tunisia [Saa 4 Usiku]

Januari 24

KUNDI D

Ghana v Botswana [Saa 1 Usiku]

Mali v Guinea [Saa 4 Usiku]

Januari 25

KUNDI A

Libya v Zambia [Saa 1 Usiku]

Equatorial Guinea v Senegal [Saa 4 Usiku]

Januari 26

KUNDI B

Sudan v Angola [Saa 1 Usiku]

Ivory Coast v Burkina Faso [Saa 4 Usiku]

Januari 27

KUNDI C

Niger v Tunisia [Saa 1 Usiku]

Gabon v Morocco [Saa 4 Usiku]

Januari 28

KUNDI D

Botswana v Guinea [Saa 1 Usiku]

Ghana v Mali

Januari 29

KUNDI A

Equatorial Guinea v Zambia [Saa 3 Usiku]

Libya v Senegal [Saa 3 Usiku]

Januari 30

KUNDI B

Sudan v Burkina Faso [Saa 3 Usiku]

Ivory Coast v Angola [Saa 3 Usiku]

Januari 31

KUNDI C

Gabon v Tunisia [Saa 3 Usiku]

Niger v Morocco [Saa 3 Usiku]

Februari 1

KUNDI D

Botswana v Mali [Saa 3 Usiku]

Ghana v Guinea [Saa 3 Usiku]

ROBO FAINALI

Februari 4

Mshindi wa Kwanza Kundi A v Mshindi wa Pili Kundi B==Mechi Namba 25

Mshindi wa Kwanza Kundi B v Mshindi wa Pili Kundi A==Mechi Namba 26

Februari 5

Mshindi wa Kwanza Kundi C v Mshindi wa Pili Kundi D==Mechi Namba 27

Mshindi wa Kwanza Kundi D v Mshindi wa Pili Kundi C==Mechi Namba 28

NUSU FAINALI

Februari 8

Mshindi Mechi Namba 25 v Mshindi Mechi Namba 28

Mshindi Mechi Namba 27 v Mshindi Mechi Namba 26

MSHINDI WA 3

Februari 11-Jijini Malabo, Equatorial Guinea

FAINALI

Februari 12-Jijini Libreville, Gabon

Kutoa maoni

Tafadhali toa maoni sahihi kwa kutumia lugha ya heshima.


Security code
Onyesha tena

Ingia

Jiandikishe / Ingia

MATANGAZO

TANGAZA_BURE2
SOKAINBONGO_BANNER1