DIMBANI AFRIKA

SH. 2,000 TU KUONA MECHI YA STARS, DRC

Jumatatu, 20 Februari 2012 16:53
Chapisha Toleo la kuchapisha

TAIFA_STARS-smallTaarifa kutoka kwa Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, Boniface Wambura imesema kiingilio kwa ajili ya mechi ya Kirafiki ya Kimataifa kati ya Taifa Stars na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) itakayofanyika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Alhamisi Februari 23 kitakuwa Sh. 2,000 kwa Viti vya Kijani na Bluu.

Eneo hilo la Viti vya Kijani na Bluu linachukua Watazamaji 36,693 ambao ni karibu theluthi mbili ya Viti vyote kwenye Uwanja huo wa kisasa.

Viti vya rangi ya Chungwa kiingilio ni Sh. 5,000, VIP C itakuwa Sh. 7,000 wakati VIP B tiketi zitauzwa kwa Sh. 10,000.

Kiingilio kwa viti vya VIP A kitakuwa Sh. 15,000.

Kwa vile Februari 23 ni siku ya kazi na ili kutoa fursa kwa Washabiki wengi kushuhudia pambano hilo la Kimataifa, mechi hiyo itaanza saa 11 kamili jioni.

Taifa Stars inayofundishwa na Jan Poulsen imeingia kambini leo na inatarajiwa kuanza mazoezi jioni hii kwenye Uwanja wa Karume na DRC ambayo iko chini ya kocha Claude Le Roy, aliewasili Nchini tangu juzi, inatarajiwa kutua Nchini kesho.

Taifa Stars na DRC zinatumia mechi hiyo kunoa Wachezaji wao kabla ya mechi zao za mchujo za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON2013) zitakazofanyika Mwakani nchini Afrika Kusini.

Katika Raundi ya Awali ambayo mechi zake zitachezwa Februari 29 mwaka huu, Stars itaanzia nyumbani dhidi ya Msumbiji wakati DRC inaanzia ugenini dhidi ya Seychelles.

 

Stars v Congo: KOCHA wa Congo atua Dar, Timu kuingia Jumanne

Jumapili, 19 Februari 2012 17:17
Chapisha Toleo la kuchapisha

TAIFA_STARS-smallKwa mujibu wa taarifa iliyosambazwa na Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, Boniface Wambura, Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Congo DR, Claude Le Roy, amewasili jana Jijini Dar es Salaam akitokea Paris, Ufaransa na Msafara kamili wa Watu 24 wakiwemo Wachezaji 19 wa Timu ya Congo DR utaingia Nchini hapo Jumanne Februari 21 kwa ajili ya Mechi yao ya Kimataifa ya Kirafiki dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam hapo Alhamisi Februari 23.

Claude Le Roy, Raia wa Ufaransa, aliteuliwa kuwa Kocha wa Congo Septemba Mwaka jana na huko nyuma aliwahi pia kuwa Kocha wa Senegal, Ghana na Cameroun.

Taarifa hiyo ya TFF pia ilisema Makocha Jan Poulsen wa Taifa Stars na Claude Le Roy watakuwa na Mkutano na Wanahabari hapo Februari 22 utakaofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya TFF.

Mechi hii na Congo DR ni ya majaribio na matayarisho kwa Taifa Stars ambao wanakabiliwa na mechi ya kuwania kutinga Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2013, zitakazochezwa huko Afrika Kusini Mwaka 2013 dhidi ya Msumbiji itakayochezwa Februari 29 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kurudiana huko Maputo hapo tarehe 17 Juni 2012.

 

Gyan astaafu Ghana!

Jumamosi, 18 Februari 2012 18:30
Chapisha Toleo la kuchapisha

ASAMOAH_GYANStraika wa Ghana Asamoah Gyan inasemekana ameamua kupumzika kuichezea Ghana baada ya kutuma barua kwa Chama cha Soka Ghana, GFA, akielezea uamuzi wake huo.

Gyan, Miaka 26, ambae ameichezea Ghana mara 59, ameleza kuwa uamuzi wake huo unatokana na kukashifiwa vibaya mara baada ya Ghana kubwagwa nje toka kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2012, hivi majuzi walipofungwa bao 1-0 na Zambia.

Mchezaji huyo amekuwa akisakamwa mno Nchini kwao kwa kuwaletea maudhi makubwa kwa kukosa penati kwenye mechi ya AFCON 2012 dhidi ya Zambia na pia kwenye Robo Fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Uruguay huko Afrika Kusini Mwaka 2010.

Barua hiyo ya Gyan imeeleza kuwa uamuzi wake hakuuchukua kwa mzaha na anasikia fahari kubwa kuichezea Ghana tangu akiwa na Miaka 17 Mwaka 2003.

Akimalizia barua yake, Gyan, ambae sasa anacheza kwa mkopo huko UAE na Klabu ya Al Ain toka Sunderland, amesema ataijulisha GFA akiamua kurudi tena kuichezea Ghana.

Gyan ameifungia Ghana bao 28 katika Mechi 59 alizoichezea.

 

DAR YAZIZIMA-Mtanange wa Yanga v Zamalek

Jumamosi, 18 Februari 2012 13:10
Chapisha Toleo la kuchapisha
Yanga_v_Zamalek

Leo Saa 10 jioni, Yanga , Mabingwa wa Soka Tanzania Bara, wanatinga Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kuivaa Zamalek ya Misri, ambao ni Mabingwa wa zamani wa Afrika waliotwaa Taji hilo mara 5, katika mechi ya Raundi ya Awali ya CAF Championz Ligi na pambano hili limeufanya Mji wote wa Dar es Salaam ujae hisia kali kwa Washabiki wa Soka huku wengine wakiwa na sikio lao huko Kigali, Rwanda ambako wakongwe wengine wa Soka Simba watakuwa wakicheza mechi yao ya kwanza ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Kiyovu ya huko.

Katika mahojiano na Wanahabari hapo jana, Kocha Msaidizi wa Zamalek, Ossama Nabil alisema wao wapo hapa si kutafuta ushindi tu bali lengo lao ni kutwaa Ubingwa wa Afrika ambao waliuchukua mara ya mwisho Mwaka 2002.

Nae Kocha wa Yanga, Kostadin Papic, ametamka: ‘Kama kocha nimemaliza kazi yangu, ninaweza kusema tupo tayari kupambana na Zamalek katika pambano hili gumu. Hatuna la zaidi uwanjani zaidi ya ushindi!’

Mbali ya wakongwe hawa Yanga na Simba, Timu za Zanzibar, Mafunzo na Jamhuri, nazo zitaingia uwanjani kwa Mafunzo kucheza na Liga Muculmana de Maputo ya Msumbiji katika CAF CHAMPIONZ LGI na Jamhuri kuivaa Hangwe ya Zimbabwe kwenye Kombe la Shirikisho.

MUNGU IBARIKI TANZANIA!

 

LIGI KUU VODACOM: Ratiba yarekebishwa kupisha Stars

Ijumaa, 17 Februari 2012 17:12
Chapisha Toleo la kuchapisha

NESHNO_MAKALA_SPESHOShirikisho la Soka Tanzania, TFF, limefanya marekebisho kwenye Ratiba ya Ligi Kuu Vodacom ili kuzipisha mechi mbili za Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, watakazocheza Wiki ijayo.

Alhamisi Februari 23, Taifa Stars watacheza mechi ya kujipima nguvu na Congo DR Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na Jumatano Februari 29 kwenye Uwanja huo huo watacheza na Msumbiji mechi ya kwanza kuwania kutinga Fainali za AFCON 2013 zitazochezwa huko Afrika Kusini Mwaka 2012.

Kwa mujibu wa Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, marekebisho ya Ratiba ya Ligi ni kutokana na makubaliano na Klabu za Ligi Kuu Vodacom kuwa pale ambapo Taifa Stars itakuwa na mechi, Ligi itasimama kupisha mechi husika.

Mechi ambazo zimebadilishwa ni zifuatazo pamoja na tarehe zake mpya:

Machi 3

JKT Ruvu v Toto African

JKT Oljoro v Kager Sugar

Machi 10

Yanga v Azam FC

Machi 7

African Lyon v Ruvu Shooting

JKT Oljoro v Toto African

Machi 11

Polisi Dodoma v Kagera Sugar

Moro United v JKT Ruvu

MSIMAMO:

TIMU

P

W

D

L

GF

GA

GD

PTS

1

Simba

17

11

4

2

27

10

17

37

2

Yanga

17

11

4

2

29

13

16

37

3

Azam

18

10

5

3

22

9

13

32

4

JKT Oljoro

17

7

5

6

10

12

-2

26

5

Mtibwa Sugar

17

7

4

6

20

17

3

25

6

JKT Ruvu

17

5

7

5

17

19

-2

22

7

Kagera Sugar

18

4

9

5

19

19

0

21

8

Coastal Union

18

7

2

9

17

20

-3

23

9

Ruvu Shooting

19

4

10

5

16

17

-1

22

10

African Lyon

16

4

5

7

15

20

-5

17

11

Moro United

18

3

8

7

22

29

-7

17

12

Villa Squad

18

4

4

10

18

35

-17

16

13

Toto African

16

2

8

6

14

20

-6

14

14

Polisi Dodoma

17

2

7

8

16

23

-7

13

 


Page 1 of 39

Ingia

Jiandikishe / Ingia

MATANGAZO

TANGAZA_BURE2
SOKAINBONGO_BANNER1