Bongo Nyuzi

KAMATI YA UCHAGUZI TFF—Yasimamisha Uchaguzi DRFA!

Jumatano, 22 Februari 2012 16:50
Chapisha Toleo la kuchapisha

Leo Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi TFF, Deaogratias Lyatto, ametoa Taarifa kuhusu Uchaguzi wa Viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam, DRFA, kufuatia kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika tarehe 21 Februari 2012 kupitia mchakato wa Uchaguzi wa DRFA na ambacho pia kilijadili ushauri wa Kamati ya Sheria, Katiba na Hadhi kwa Wachezaji kuhusu Katiba ya DRFA.

NATIONAL_STADIUM2Taarifa hiyo inasema: ‘Kamati iliridhika na kukubaliana na ushauri wa Kamati ya Sheria, Katiba na Hadhi kwa Wachezaji kwamba Katiba ya DRFA haikidhi matakwa ya Katiba ya TFF.’

Taarifa hiyo iliendelea: ‘Kutokana na mapungufu ya msingi katika Ibara ya 29 na Ibara ya 30 ya Katiba ya DRFA, Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuzingatia Katiba ya TFF Ibara ya 49(1), Katiba ya DRFA Ibara ya 48, na Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF Ibara ya 26(2), Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kutumia mamlaka yake kikatiba na kikanuni imefuta uchaguzi wa DRFA uliokuwa ufanyike tarehe 18 Machi 2012. Mchakato wa Uchaguzi wa DRFA utaanza upya mara baada ya kukamilika marekebisho ya Vifungu vya Katiba ya DRFA vinavyokinzana na matakwa ya Katiba ya TFF kwa maelekezo ya Kamati ya Sheria, Katiba na Hadhi kwa Wachezaji, kabla ya tarehe 10 Agosti 2012.’

Taarifa hiyo ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilimalizia kwa kusema: ‘Kamati ya Uchaguzi ya TFF inatabaisha kuwa kwa kuzingatia Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF Ibara ya 2(4), uongozi wa DRFA utaendelea kuwa madarakani hadi hapo uchaguzi utakapofanyika kabla ya tarehe Agosti 2012 muda wao kuwa madarakani kikatiba utakapomalizika.’

Kutoa maoni

Tafadhali toa maoni sahihi kwa kutumia lugha ya heshima.


Security code
Onyesha tena

Ingia

Jiandikishe / Ingia

adidas

All Originals 300x250

MATANGAZO

TANGAZA HAPA

All Originals 728x90