Bongo Nyuzi

CAF AFRIKA: Simba, Yanga-WOTE NGOMA NGUMU!

Jumamosi, 18 Februari 2012 20:02
Chapisha Toleo la kuchapisha
YANGA_V_SIMBA11

Vigogo wa Soka Tanzania, Yanga na Simba, leo zimeanza kampeni zao katika michuano ya Klabu Barani Afrika kwa kutoka sare ya bao 1-1 katika mechi zao zilizochezwa leo.

Yanga, wakiwa Dar es Salaam Uwanja wa Taifa wakicheza mechi ya CAF CHAMPIONZ LIGI dhidi ya Zamalek ya Misri, walitangulia kupata bao dakika ya 36 mfungaji akiwa Hamisi Kiiza lakini Zamalek ilisawazisha kipindi cha pili dakika ya 74 kwa bao la Straika wao wanaemwita ‘buldoza’ Amr Zaki.

Timu hizi zimepangwa kurudiana hapo Machi 3 lakini hadi sasa haijulikani mechi hiyo kama itachezwa na ikichezwa basi wapi itachezwa maana Soka la Misri limesimamishwa baada ya maafa ya kufa Watu 74 uwanjani baada ya mechi kati ya Klabu za Al-Masry na Al-Ahly hivi karibuni mkasa ambao uliifanya Serikali ya Misri iwatimue Viongozi wote wa Soka na hili kuifanya FIFA itake Viongozi hao warudishwe mara moja.

Hadi sasa si CAF wala FIFA imezungumzia lolote nini hatima ya Soka la Misri kwani kuingiliwa Soka na Serikali ni kinyume cha kanuni za FIFA na ikitokea hivyo Nchi husimamishwa hadi Viongozi halali warudishwe.

Nako toka huko Kigali, Rwanda leo Simba ilitoka sare ya bao 1-1 na Kiyovu katika mechi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho na bao la Simba kufungwa na Mwinyi Kazimoto lakini Kiyovu walisawazisha dakika za mwishoni.

MATOKEO MECHI NYINGINE ZA LEO:

CAF CHAMPIONS LIGI

Tusker [Kenya] 0 APR FC [Rwanda] 0

URA [Uganda] 3 Correction Services [Lesotho]

Foullah Edifice [Chad] 0 JSM Bejais [Algeria] 0

KOMBE LA SHIRIKISHO

Black Leopards [South Africa] 1 Motor Action FC 1 [Zambia]

Nania FC [Ghana] 0 FS Sequence 3 [Guinea] 3

Red Arrows [Zambia] 0 Royal Leopards 0 [Swaziland]

Maoni 

 
0 # Handsomeboy 2012-02-18 21:02
Site yako http://sokainbongo.com ni nzuri ila kwa sisi tunaotumia simu inakuwa kubwa sana inatumia mb 400 hadi 500 kwenye kuifungua tu. Kama hujanielewa test kuingia www.sokainbongo.com kwa kutumia simu uone inavyozingua ni tofauti kabsa na site zingine kama vile www.shaffihdauda.com. Fanya mpango uiboreshe iwe simple hata kwa watumiaji wa simu. kwa sisi fans wako tunaotumia simu tunateseka hadi tunaona uvivu hata kuingia kwenye www.sokainbongo.com.
+++++++++++++++ ++++++++++++
SHUKRAN Handsomeboy,
Tutafanyia kazi hili.
SOKA in BONGO
Reply | Reply with quote | Quote
 

Kutoa maoni

Tafadhali toa maoni sahihi kwa kutumia lugha ya heshima.


Security code
Onyesha tena

Ingia

Jiandikishe / Ingia

adidas

All Originals 300x250

MATANGAZO

TANGAZA HAPA