MATOKEO:
Jumatano Februari 15
Jkt Oljoro 0 Ruvu Shooting 1
Azam FC 4 Villa Squad 1
Coastal Union 2 JKT Ruvu 0
Kagera Sugar 2 Moro United 2
TAARIFA:
Jana huko Uwanja wa Chamazi, wenyeji Azam FC waliwatandika Villa Squad bao 4-1 katika mechi ya Ligi Kuu Vodacom na kuwanyemelea Vigogo walio kileleni Simba na Yanga na kuwa pointi mbili nyuma yao.
Sasa, Azam waliocheza mechi moja zaidi ya Vigogo hao, wana pointi 35 na Simba na Yanga zina pointi 37 kila mmoja.
Villa Squad walitangulia kupata bao mfungaji akiwa Nsa Job lakini Azam wakasawazisha kwa bao la Salum Abukari na mengine kufungwa na Abdi Kassam, Khamis Mcha na Kipre Tchetche.
Mechi hii ilitawaliwa na ghasia na kusababisha Polisi kufyatua mabomu ya machozi ili kudhibiti rabsha hizo.