Bongo Nyuzi

Papic hana furaha

Jumanne, 14 Februari 2012 12:33
Chapisha Toleo la kuchapisha

YANGA++Majeruhi pia wamkera!

Kocha wa Yanga, Kostadin Papic, anakerwa na kiwango cha Timu yake licha ya juzi kuifunga Ruvu Shooting bao 1-0 katika mechi ya Ligi Kuu Vodacom iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambayo iliwafanya iwakamate Simba kwa pointi kileleni.

++++++

MSIMAMO Timu za juu LIGI KUU VODACOM:

1 Simba Pointi 37 [Bao za kufunga 27, kufungwa 10, tofauti ya Magoli 17]

2 Yanga Pointi 37 [Bao za kufunga 29, kufungwa 13, tofauti ya Magoli 16]

3 Azam Pointi 32

3 JKT Oljoro Pointi 26

5 Mtibwa Sugar Pointi 22

++++++

Huku wakikabiliwa na mechi ngumu ya CAF Championz Ligi na Zamalek ya Misri itakayochezwa Jumamosi Februari 18 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Papic amekiri Timu yake haipo tayari na hawezi kuahidi ushindi hasa kwa vile Wachezaji wake hawana umakini katika kufuata maelekezo wanayopewa.

Mbali ya hilo, Papic pia amekiri majeruhi wengi wanaathiri na amewataja majeruhi hao kuwa ni Rashid Gumbo, Salum Telela, Nurdin Bakari na Godfrey Bonny lakini amefurahishwa na kurejea kundini kwa Nahodha wake Shadrack Nsajigwa ambae alikuwa kwenye kifungo cha mechi 3 baada ya kutolewa kwa Kadi Nyekundu walipocheza na Moro United.

Kocha huyo pia ameshauri kuwa kwa vile muda uliobakia ni mchache wasisumbuke kuihamishia kambi yao ya mazoezi nje ya Dar es Salaam.

Kutoa maoni

Tafadhali toa maoni sahihi kwa kutumia lugha ya heshima.


Security code
Onyesha tena

Ingia

Jiandikishe / Ingia

adidas

All Originals 300x250

MATANGAZO

Adidas Predator 300x250

TANGAZA HAPA

All Originals 728x90