Taarifa:
RATIBA:
Jumamosi Februari 11
Coastal Union v African Lyon
JKT Oljoro v JKT Ruvu
Polisi Dodoma v Villa Squad
Simba v Azam
Toto African v Moro United
MSIMAMO Timu za juu:
[Kila Timu imecheza Mechi 16]
1 Yanga Pointi 34 [Bao za kufunga 28, kufungwa 13, tofauti ya Magoli 15]
2 Simba Pointi 34 [Bao za kufunga 25, kufungwa 10, tofauti ya Magoli 15]
3 Azam Pointi 32
3 JKT Oljoro Pointi 26
5 Mtibwa Sugar Pointi 22
Taarifa:
Ligi Kuu Vodacom leo inaendelea huku mechi yenye mvuto mkubwa ni ile itakayochezwa Uwanja wa Taifa kati ya Simba iliyo nafasi ya pili kucheza na Azam FC walio nafasi ya 3.
Mara ya mwisho Timu hizi kukutana ilikuwa Mwezi Januari huko Zanzibar kwenye Mapinduzi Cup na Simba kunyukwa 2-0 na Azam.
Katika mechi ya leo Simba wanatarajiwa kumchezesha Felix Sunzu ambae hajacheza hata mechi moja za raundi ya pili ya Ligi kwa sababu ya kuumia na nao Azam wana nafasi kumtumia kwa mara ya kwanza Mchezaji wao kutoka Ivory Coast Balou Tchetche ambae ameshabarikiwa na TFF baada ya kupata Hati ya Uhamisho wa Kimataifa.
Mbali ya mechi ya Simba na Azam leo pia zipo mechi nyingine ambazo ni kati ya Toto Africans na Moro United (Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza), Polisi Dodoma na Villa Squad (Uwanja wa Jamhuri, Dodoma), Coastal Union na African Lyon (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga) na JKT Oljoro na JKT Ruvu (Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha).
MICHUANO YA CAF, YANGA NA SIMBA ZAGOMEWA
Shirikisho la Kandana la Tanzania, TFF, limesema kuwa yale maombi yao kutaka mechi za Yanga na Simba kwenye michuano ya Afrika zisogezwe mbele kwa vile zipo karibu na mechi ya Taifa Stars na Msumbiji kuwania kuingia Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2013, zitakazochezwa huko Afrika Kusini, yamekataliwa.
Taifa Stars na Msumbiji wanatarajiwa kucheza Februari 29 na zile mechi za Yanga na Simba za CAF zipo Wikiendi ya Machi 2, 3 na 4 wakati Simba watakapokuwa Dar es Salaam kurudiana na Kiyovu na Yanga watakuwa huko Cairo kurudiana na Zamalek.
Akiongelea kutupwa maombi hayo, Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, alisema: ‘CAF ilikuwa tayari kuridhia maombi hayo iwapo Chama cha Mpira wa Miguu cha Misri (EFA) na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Rwanda (FERWAFA) wangekubali, lakini EFA na FERWAFA wamekataa ombi hilo kwa vile litavuruga ratiba ya mechi za ligi katika nchi hizo.’
Hata hivyo mechi ya Zamalek na Yanga huko Cairo ipo kwenye hatihati kwa vile shughuli zote za Soka huko Misri zimesimamishwa kufuatia vifo vya Watu 74 Uwanjani baada ya mechi kati ya Al-Masry na Al-Ahly huko Mjini Port Said kitu kilichoifanya Serikali ya Misri kuwatimua Viongozi wa Soka wa EFA na ambacho kimepingwa na FIFA ambao wametaka Viongozi hao warudishwe.
RATIBA MECHI ZIJAZO ZA LIGI:
Jumapili Februari 12
Kagera Sugar v Mtibwa Sugar
Yanga v Ruvu Shooting [Itachezwa Uwanja wa Taifa badala ya Chamazi, Dar es Salaam]
Jumapili Februari 13
Kagera Sugar v Mtibwa Sugar
Jumanne Februari 14
Polisi Dodoma v Simba
Yanga v African Lyon
Jumatano Februari 15
Toto Africans v Mtibwa Sugar