MSIMAMO:
-Simba Pointi 31
-Yanga 28
-Azam FC 26
==========
Katika mechi za Ligi Kuu Vodacom zilizochezwa jana Jijini Dar es Salaam kwenye Viwanja viwili tofauti, vinara wa Ligi Simba waliendelea kugangamala kileleni pale walipoichapa Coastal Union ya Tanga bao 2-1 kwenye mechi iliyochezwa Uwanja wa Taifa na huko Chamazi Azam FC pia walishinda 2-1 dhidi ya African Lyon.
Simba ndio waliotangulia kupta bao kwenye Uwanja wa Taifa baada ya Haruna Moshi ‘Boban’ kuunganisha krosi ya Shomari Kapombe katika dakika ya 41.
Bao la pili la Simba lilifungwa na Davies Kago katika dakika ya 81 na Coastal Union kupata bao lao moja dakika mbili baadae kwa penati ya Hamisi Shengo.
Huko Chamazi, Wenyeji Azam FC walishinda 2-1 kwa bao za Hassan Mwamba wa African Lyon, aliejifunga mwenyewe, na John Bocco.
Bao la Lyon lilifungwa na Sammy Kesi.
