Mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga, wamepewa Siku 30 na FIFA kumlipa Mchezai wao wa zamani kutoka Kenya John Njoroge Shilingi Milioni 17,159,800/= ama watachukuliwa hatua.
Habari kuhusu uamuzi wa FIFA zimethibitishwa na TFF ambao wamesema kuwa FIFA iliridhika kuwa Yanga ilivunja Mkataba na Mchezaji huyo kinyume cha taratibu.
Yanga imetakiwa itoe malipo hayo ndani ya Siku 30 na ikichelewa itatozwa riba ya asilimia 5 ya fedha hizo pamoja na kuchukuliwa hatua za ziada.
Sakata hili la Njoroge, ambae sasa yupo na Klabu ya Kenya Sofapaka, lilianza Miaka miwili iliyopita wakati Mchezaji huyo pamoja wenzake Ally Msigwa, Steven Malashi na Wisdom Ndhlovu, toka Malawi, walipotemwa na wao wakalalamika kwa SPUTANZA [Soccer Players Union of Tanzania], Chama cha Kutetea Haki za Wachezaji wa Tanzania ambacho kupitia Katibu Mkuu wake, Said George, kilipeleka malalamiko kwa TFF wakidai Wachezaji hao wamekatishiwa Mikataba yao kinyume cha makubaliano.

Maoni