Bongo Nyuzi

Yanga yampa onyo Papic ‘kubwabwaja’ na Wanahabari!

Jumanne, 24 Januari 2012 22:41
Chapisha Toleo la kuchapisha

YANGA_JUUUMabingwa wa Ligi Kuu Vodacom, Yanga, wamemuonya Kocha wao Mkuu Kostadin Papic kuacha kuongea na kulalamika kwenye Vyombo vya Habari bila Uongozi wa Klabu kujua.

Onyo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Yanga, Lloyd Nchunga, ambae amesema wamemwandikia barua Kocha huyo kutoka Serbia kuacha kuzungumza mambo ya ndani ya Klabu na Waandishi wa Habari na badala yake aongee na Uongozi kwanza.

Hivi karibuni iliripotiwa Kocha huyo aliongea na Wanahabari akilalamikia maandalizi duni ya Timu kwa ajili ya raundi ya pili ya Ligi Kuu na mechi ya CAF CHAMPIONZ LIGI dhidi ya miamba wa Egypt Zamalek na pia kupinga kupigwa kambi ya mazoezi huko Mjini Mwanza.

Lakini Nchunga alishangazwa na hatua hiyo kwani Papic alipendekeza Timu iende kupiga kambi Afrika Kusini na Uongozi ulimkubalia na kumtaka atume ripoti kwao kuhusu mpango huo lakini alishindwa na ndipo wao wakaamua wapeleke Timu Mwanza.

Yanga itakuwa huko Mwanza hadi itakaporudi Dar es Salaam kwa ajili ya mechi na Zamalek itakayochezwa Uwanja wa Taifa Februari 18.

Kutoa maoni

Tafadhali toa maoni sahihi kwa kutumia lugha ya heshima.


Security code
Onyesha tena

Ingia

Jiandikishe / Ingia

MATANGAZO

TANGAZA_BURE2