Bongo Nyuzi

Yanga yanasa kwa Moro United

Jumapili, 22 Januari 2012 08:08
Chapisha Toleo la kuchapisha

YANGA_LOGO[Habari hizi zimechangiwa pia na Petronas Akili]

MATOKEO:

%1 JAN. 2012

Moro United 2 Yanga 2

Mtibwa Sugar 0 JKT Oljoro 1 Ruvu Shooting 2 Toto African 0

Villa Squad 2 Kagera Sugar 4

JKT Ruvu v Polisi Dodoma

TAARIFA:

Yanga jana walishindwa kuipiku Simba toka kileleni baada ya kulazimishwa sare ya bao 2-2 na Moro United katika mechi ya kwanza ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Vodacom iliyochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Yanga walilazimika kucheza mechi hii kwa muda mrefu wakiwa Mtu 10 baada ya Beki wao Shadrak Na kucheza mechi hii kwa muda mrefu wakiwa Mtu 10 baada ya Beki wao Shadrak Nsajigwa kutolewa kwa Kadi Nyekundu kwenye Kipindi cha Kwanza kwa kile kilichodaiwa kumpiga kipepsi Mchezaji wa Moro United.

Lakini Yanga ndio waliotangulia kufunga bao mfungaji akiwa Kenneth Asamoah kutoka Ghana na bao hilo lilidumu hadi mapumziko.

Kipindi cha pili Moro United walisawazisha na kufunga bao la pili kwa bao za Benedict Ngasa na Simon Msuya.

Yanga walipata bao lao la pili la kusawazisha kwa penati ya Hamis Kiiza na wangeweza hata kushinda ingekuwa wako makini walipofika langoni.

RATIBA:

25 Jan. 2012

African Lyon vs Azam FC [Chamazi Dar es salaam]

Simba v Coastal Union Uwanja wa Taifa Dar es salaam]

Kutoa maoni

Tafadhali toa maoni sahihi kwa kutumia lugha ya heshima.


Security code
Onyesha tena

Ingia

Jiandikishe / Ingia

MATANGAZO

TANGAZA_BURE2