Ligi Kuu Bara, rasmi kama Ligi Kuu Vodacom, inarudi tena kilingeni kuanza mzunguko wake wa pili Wikiendi hii toka mapumziko ya karibu Miezi mitatu huku Wakongwe Simba, wakiwa kileleni, Mabingwa Yanga wakiwa nafasi ya pili na ‘Timu Tajiri’ Azam FC, Timu ambayo hivi majuzi ilizitwanga Yanga na Simba na kutwaa Mapinduzi Cup huko Zanzibar, ikiwa nafasi ya 3.
Baada ya mechi 13 kwa kila Timu, Simba wako juu wakiwa na Pointi 28, Yanga ni wa pili na wana wana Pointi 27 na inafuatia Azam FC yenye pointi 24 wakiwa wamefungana na JKT Oljoro.
Mkiani wapo Villa Squad wenye Pointi 7.
Katika raundi hii, Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, limeamua kuwa mechi za Ligi zitakuwa zikichezwa katika Siku tatu tu za Wiki ambazo ni Jumamosi, Jumapili na Jumatano badala ya ile shagalabagala ya mzunguko wa kwanza.
Yanga wataanza mzunguko wa pili kwa kucheza Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam dhidi ya Moro United hapo Jumamosi Januari 21 na watani zao Simba wataingia dimbani Jumatano Januari 25 Uwanja huo huo kucheza na wapwa zao toka Tanga Coastal Union.
Nao Azam FC wataanzia mzunguko wa pili nyumbani kwao Chamazi kwa kucheza na African Lyon hapo Jumatano Januari 25.
RATIBA:
Januari 21:
Ruvu Shooting v Toto African [Mlandizi, Pwani]
Villa Squad v Kager Sugar [Chamazi, Dar es Salaam]
Yanga v Moro United [Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam]
Mtibwa Sugar v JKT Oljoro [Manungu, Morogoro]
Januari 22
JKT Ruvu v Polisi Dodoma [Chamazi, Dar es Salaam]
Januari 25
Simba v Coastal Union [Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam]
Azam FC v African Lyon [Chamazi, Dar es Salaam]
Januari 28
Villa Squad v Toto African [Chamazi,Dar es Salaam]
JKT Ruvu v Yanga [Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam]
Ruvu Shooting v Kagera Sugar [Mlandizi, Pwani]
Januari 29
Moro united v Azam FC [Chamazi, Dar es Salaam]
Mtibwa Sugar v Coastal Union [Manungu, Morogoro]
Februari 1
Simba v JKT Oljoro [Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam]
African Lyon v Polisi Dodoma [Chamazi, Dar es Salaam]
