Makocha wa Klabu kongwe Nchini, Yanga na Simba, ambao Timu zao zinakabiliwa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara utakaoanza hapo Januari 21 na pia Mashindano ya Klabu za Afrika Mwezi Februari, wameonyesha kutoridhika na Vikosi vyao wakati wakijifua kwa michuano hiyo.
Kocha wa Simba, Milovan Cirkovic, amekaririwa akisema kiwango cha Timu yake na hasa safu ya ulinzi bado hakiridhishi.
Majuzi Simba walitoka sare 1-1 na Tusker ya Kenya na Cirkovic alionekana kutofurahishwa na uchezaji wa Timu yake.
Simba inatarajiwa kucheza michuano ya Afrika ya Kombe la Shirikisho ugenini Kigali, Rwanda ambapo itamenyana na Kiyovu ya huko Februari 18 katika mechi ya kwanza.
Nae Kocha wa Yanga, Kostadin Papic, ameponda matayarisho ya Timu kwa kukumbwa na kuvunjika kwa mazoezi na kambi yao kukabiliwa na matatizo mengi.
