BONGO NYUZI

KAMATI YA UCHAGUZI TFF—Yasimamisha Uchaguzi DRFA!

Jumatano, 22 Februari 2012 16:50
Chapisha Toleo la kuchapisha

Leo Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi TFF, Deaogratias Lyatto, ametoa Taarifa kuhusu Uchaguzi wa Viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam, DRFA, kufuatia kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika tarehe 21 Februari 2012 kupitia mchakato wa Uchaguzi wa DRFA na ambacho pia kilijadili ushauri wa Kamati ya Sheria, Katiba na Hadhi kwa Wachezaji kuhusu Katiba ya DRFA.

NATIONAL_STADIUM2Taarifa hiyo inasema: ‘Kamati iliridhika na kukubaliana na ushauri wa Kamati ya Sheria, Katiba na Hadhi kwa Wachezaji kwamba Katiba ya DRFA haikidhi matakwa ya Katiba ya TFF.’

Taarifa hiyo iliendelea: ‘Kutokana na mapungufu ya msingi katika Ibara ya 29 na Ibara ya 30 ya Katiba ya DRFA, Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuzingatia Katiba ya TFF Ibara ya 49(1), Katiba ya DRFA Ibara ya 48, na Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF Ibara ya 26(2), Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kutumia mamlaka yake kikatiba na kikanuni imefuta uchaguzi wa DRFA uliokuwa ufanyike tarehe 18 Machi 2012. Mchakato wa Uchaguzi wa DRFA utaanza upya mara baada ya kukamilika marekebisho ya Vifungu vya Katiba ya DRFA vinavyokinzana na matakwa ya Katiba ya TFF kwa maelekezo ya Kamati ya Sheria, Katiba na Hadhi kwa Wachezaji, kabla ya tarehe 10 Agosti 2012.’

Taarifa hiyo ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilimalizia kwa kusema: ‘Kamati ya Uchaguzi ya TFF inatabaisha kuwa kwa kuzingatia Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF Ibara ya 2(4), uongozi wa DRFA utaendelea kuwa madarakani hadi hapo uchaguzi utakapofanyika kabla ya tarehe Agosti 2012 muda wao kuwa madarakani kikatiba utakapomalizika.’

 

TAARIFA TOKA TFF: Wanachama TFF watakiwa kurekebisha Katiba

Jumanne, 21 Februari 2012 17:19
Chapisha Toleo la kuchapisha

NATIONAL_STADIUM2Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, leo limetoa taarifa kwamba Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya TFF ilikutana Februari 15 Mwaka huu Jijini Dar es Salaam na kufanya uamuzi kwa ajenda mbalimbali ikiwemo Marekebisho ya Katiba za Wanachama wa TFF na pia ushauri wa kisheria ulioombwa kwake na Kamati ya Uchaguzi ya TFF.

Kikao hicho kiliamua kwamba Wanachama wake wote 40 wa TFF wanatakiwa kufanya marekebisho kwenye Katiba zao katika maeneo matatu kwa mujibu wa maelekezo ambayo TFF ilitoa Mwaka jana.

Maeneo ambayo yanatakiwa kurekebishwa ni sifa za Wagombea uongozi ambapo kwenye kipengele cha elimu ni lazima iwe kuanzia Kidato cha Nne, kutopeleka masuala ya Soka Mahakama za kawaida na Kamati zao za Uchaguzi kutakiwa kufanya kazi chini ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF.

Kwa kuzingatia hayo TFF imeamua kuwa hakuna mwanachama yeyote wa TFF anaeruhusiwa kufanya Uchaguzi kwa sasa kama Katiba yake ina upungufu au inakwenda kinyume na maelekezo kuhusu maeneo hayo matatu.

Kamati hiyo imetoa hadi Juni Mosi Mwaka huu kwa Wanachama ambao Katiba zao zina upungufu katika maeneo hayo wawe wamefanya marekebisho ndiyo waendelee na Uchaguzi kwa wale ambao muda wa uchaguzi umefika.

Pia, Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji imeishauri Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwamba Katiba zote za Wanachama ziwe na vitu hivyo vitatu vilivyotakiwa kufanyiwa marekebisho.

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI- MACHI 8

Wakati huohuo TFF imetangaza kuwa Machi 8 kila mwaka ni Siku ya Wanawake Dunia na ili kuadhimisha siku hiyo kwa upande wa Soka, TFF kwa kushirikiana na Chama cha Mpira wa Miguu cha Wanawake (TWFA) imeandaa Mashindano mafupi kwa Shule nane za Sekondari za Mkoa wa Dar es Salaam.

Mashindano yataanza Februari 24 Mwaka huu kwenye Viwanja viwili vya Jitegemee Sekondari ambapo kutakuwa na Kundi B wakati kundi A litacheza mechi zake Makongo Sekondari.

Mechi zitaanza saa 8 mchana na kumalizika saa 10 jioni.

Kundi A lina shule za Makongo, Goba, Twiga na Lord Barden wakati Jitegemee, Benjamin Mkapa, Kibasila na Tiravi zitakuwa kundi B.

Kwa mujibu wa TFF, lengo la Mashindano hayo ni kuhamasisha Soka kwa Wasichana katika ngazi ya Shule, kuandaa, kubaini na kuendeleza mafanikio yanayopatikana katika Timu ya Wanawake ya Taifa.

 

CAF AFRIKA: Simba, Yanga-WOTE NGOMA NGUMU!

Jumamosi, 18 Februari 2012 20:02
Chapisha Toleo la kuchapisha
YANGA_V_SIMBA11

Vigogo wa Soka Tanzania, Yanga na Simba, leo zimeanza kampeni zao katika michuano ya Klabu Barani Afrika kwa kutoka sare ya bao 1-1 katika mechi zao zilizochezwa leo.

Yanga, wakiwa Dar es Salaam Uwanja wa Taifa wakicheza mechi ya CAF CHAMPIONZ LIGI dhidi ya Zamalek ya Misri, walitangulia kupata bao dakika ya 36 mfungaji akiwa Hamisi Kiiza lakini Zamalek ilisawazisha kipindi cha pili dakika ya 74 kwa bao la Straika wao wanaemwita ‘buldoza’ Amr Zaki.

Timu hizi zimepangwa kurudiana hapo Machi 3 lakini hadi sasa haijulikani mechi hiyo kama itachezwa na ikichezwa basi wapi itachezwa maana Soka la Misri limesimamishwa baada ya maafa ya kufa Watu 74 uwanjani baada ya mechi kati ya Klabu za Al-Masry na Al-Ahly hivi karibuni mkasa ambao uliifanya Serikali ya Misri iwatimue Viongozi wote wa Soka na hili kuifanya FIFA itake Viongozi hao warudishwe mara moja.

Hadi sasa si CAF wala FIFA imezungumzia lolote nini hatima ya Soka la Misri kwani kuingiliwa Soka na Serikali ni kinyume cha kanuni za FIFA na ikitokea hivyo Nchi husimamishwa hadi Viongozi halali warudishwe.

Nako toka huko Kigali, Rwanda leo Simba ilitoka sare ya bao 1-1 na Kiyovu katika mechi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho na bao la Simba kufungwa na Mwinyi Kazimoto lakini Kiyovu walisawazisha dakika za mwishoni.

MATOKEO MECHI NYINGINE ZA LEO:

CAF CHAMPIONS LIGI

Tusker [Kenya] 0 APR FC [Rwanda] 0

URA [Uganda] 3 Correction Services [Lesotho]

Foullah Edifice [Chad] 0 JSM Bejais [Algeria] 0

KOMBE LA SHIRIKISHO

Black Leopards [South Africa] 1 Motor Action FC 1 [Zambia]

Nania FC [Ghana] 0 FS Sequence 3 [Guinea] 3

Red Arrows [Zambia] 0 Royal Leopards 0 [Swaziland]

 

CAF AFRIKA: Yanga v Zamalek; Kiyovu v Simba

Ijumaa, 17 Februari 2012 20:10
Chapisha Toleo la kuchapisha

YANGA_V_SIMBA11Klabu kongwe Nchini, Yanga na Simba, wikiendi hii zinajimwaga dimbani kwenye Mashindano makubwa Barani Afrika huku Yanga wakiikaribisha Zamalek ya Misri Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam hapo Jumamosi kwa pambano la Raundi ya Awali ya CAF CHAMPIONZ LIGI na Simba kucheza ugenini, pia Jumamosi, huko Kigali, Rwanda na Kiyovu kwenye Kombe la Shirikisho.

Mbali ya wakongwe hawa, Timu za Zanzibar, Mafunzo na Jamhuri, nazo zitaingia uwanjani kwa Mafunzo kucheza na Liga Muculmana de Maputo ya Msumbiji katika CAF CHAMPIONZ LGI na Jamhuri kuivaa Hangwe ya Zimbabwe kwenye Kombe la Shirikisho.

Tayari Zamalek, ambao wamewahi kuwa Mabingwa wa Afrika mara 5, wameshatua Dar es Salaam bila ya Wachezi wao Ahmed Hassan, Muhammad Ibrahim na Salah Suleiman.

Majuzi Zamalek walicheza mechi yao ya mwisho ya majaribio na kuifunga Telecom Egypt bao 4-1 kwa bao za Amr Zaki, Ibrahim Hassan na Ahmad Jaffar.

Simba yaenda Rwanda bila Wachezaji kadhaa

Simba iliondoka Alhamisi jioni kwenda Kigali, Rwanda kupambana na Kiyovu huku Wachezaji kadhaa wakiachwa.

Wachezaji ambao hawakusafiri ni Gervais Kargo, Derrick Walulya, Haruna Moshi 'Boban', Ulimboka Mwakingwe, Amir Maftah na Hassan Khatib na imesemwa baadhi yao ni majeruhi.

Pamoja na Kocha Cirkovic Milovan na Wasaidizi wake Amatre, Daktari Cosmas Kapinga na James Kisaka, Kocha wa Makipa, Viongozi wengine ambao wamo kwenye msafara huo ni Makamu Mwenyekiti Geofrey Nyange 'Kaburu', Katibu mkuu Evodius Mtawala, Fransis Silaya (Mjumbe wa Kamati ya Utendaji).

Wachezaji waliosafiri ni:

Makipa: Juma Kaseja na Ali Mustapha 'Barthez'

Mabeki: Nassor Said 'Cholo', Juma Jabu, Juma Nyoso, Kelvin Yondan, Victor Costa na Obadia Mungusa.

Viungo: Shomari Kapombe, Mwinyi Kazimoto, Jonas Mkude na Patric Mafisango Washambuliaji: Ramadhani Singano 'Messi', Edward Christopher, Salum Machaku, Uhuru Selemani, Felix Sunzu na Emmanuel Okwi.

 

POULSEN ATAJA STARS WA MSUMBIJI

Alhamisi, 16 Februari 2012 17:45
Chapisha Toleo la kuchapisha

JAN_POULSENKocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Jan Poulsen, ametangaza majina ya Wachezaji 23 watakaoingia kambini kujitayarisha kwa mechi ya mchujo kutinga Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2013, zitakazochezwa huko Afrika Kusini Januari Mwakani dhidi ya Msumbiji itakayochezwa Dar es Salaam hapo Februari 29.

Kikosi hicho ambacho kitaingia kambini Februari 20 kina Wachezaji wapya wawili ambao ni Jonas Gerald wa Simba na Salum Abubakar wa Azam.

Kikosi hicho cha Taifa Stars inategemewa kucheza mechi ya kirafiki ya Kimataifa na Congo DR Februari 23 Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Kikosi kamili:

Makipa: Shabani Kado [Yanga], Juma Kaseja [Simba], Mwadini Ali [Azam]

Mabeki: Shadrack Nsajigwa [Yanga], Masoud Cholo [Simba], Aggrey Morris [Azam], Juma Nyosso [Simba], Juma Jabu [Simba], Stephen Mwasika [Yanga], Kelvin Yondani [Simba]

Viungo: Jonas Gerrard [Simba], Shaban Nditi [Mtibwa Sugar], Shomari Kapombe [Simba], Salum Abubakar [Azam], Mwinyi Kazimoto [Simba] Abdi Kassam [Azam]

Mafowadi: Hussein Javu [Mtibwa Sugar], John Bosco [Azam], Nizar Khalfan [Philadelphia Union, Marekani], Mrisho Ngassa [Azam], Ally Badru Ally [Canal Suez, Misri], Uhuru Selemani [Simba], Nsa Job [Villa Squad].

 


Page 1 of 80

Ingia

Jiandikishe / Ingia

MATANGAZO

TANGAZA_BURE2