AFCON 2013-RATIBA & MATOKEO
Jumatano, 04 Januari 2012 16:38
CAF imetoa Ratiba ya Mechi za kutafuta Nchi 15 zitakazoingia Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazochezwa Mwaka 2013 huko Afrika Kusini na Tanzania imepangwa kucheza na Msumbiji kwenye Raundi ya Pili ya Mchujo. Raundi ya Pili ya Mchujo itatoa Timu 14 zitakazosonga Raundi ya Mwisho ambayo pia itajumuisha Nchi 16 zilizoshiriki Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika za 2012 huko Equatorial Guinea na Gabon kuanzia Januari 21. Raundi ya Mwisho itajumuisha Timu 30 zitakazopangwa katika Mechi 15 zitakazochezwa nyumbani na ugenini na Washindi 15 watajumuika na Wenyeji Afrika Kusini kucheza Fainali. Kawaida Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika huchezwa kila baada ya Miaka miwili lakini CAF iliamua kuwa baada ya Fainali za 2012 Mashindano hayo yasiwe yanachezwa Mwaka mmoja na Fainali za Kombe la Dunia. Fainali zijazo za Kombe la Dunia ni Mwaka 2014 huko Brazil, 2018 huko Urusi na 2022 huko Qatar na CAF itakuwa ikifanya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika Mwaka 2013 huko Afrika Kusini na Fainali zitakazofuata zitakuwa 2015, 2017, 2019, 2021 na kadhalika. Jumla ya Nchi 46 zitashiriki kinyang’anyiro hicho ili kupata Nchi 15 kujumuika na Wenyeji Afrika Kusini kwenye Fainali. TAREHE ZA MECHI: -RAUNDI YA 1: 6-8 Januari 2012 na marudiano 20-22 Januari -RAUNDI YA 2: 29 Februari 2012 na marudiano 15-17 Juni 2012 -RAUNDI YA 3: 7-9 Septemba 2012 na marudiano 12-14 Oktoba 2012 RATIBA: Raundi ya Kwanza ya Mchujo: Seychelles v Swaziland [Swaziland walijitoa] Sao Tome 1 Lesotho 0 [Mechi Namba 2] Lesotho 0 Sao Tome 0 [Sao Tome wasonga] Raundi ya Pili ya Mchujo: [Mechi kuchezwa Tarehe 29 Februari na marudiano ni Juni 15] Ethiopia 0 Benin 0 Rwanda 0 Nigeria 0 Congo 3 Uganda 1 Burundi 2 Zimbabwe 1 Kenya 2 Togo 1 Sao Tome 0 Sierra Leone 0 Chad 3 Malawi 2 Seychelles 0 DR Congo 4 Tanzania 1 Mozambique 1 Central Africa v Egypt [IMEAHIRISHWA] Madagascar 0 Cape Verde 4 Liberia 1 Namibia 0 Gambia 1 Algeria 2 Guinea Bissau 0 Cameroon 1 [Marudiano Juni 15] Kutoa maoni
|
|
|